Loading...
 

Mashindano ya Hotuba za Vichekesho

 

Vietnam 4084327 960 720

 

Muda wa Hotuba

Mashindano ya Hotuba za Vichekesho yana lengo la kutafuta wachekeshaji na waburudishaji bora.

Hotuba zinazoingia kwenye Mashidano ya Hotuba za Vichekesho hazitakiwi kuzidi muda wa dakika 7.


Uchaguzi wa Majaji

Kwa mashindano ya ngazi ya nchi na juu, majaji watakuwa sio wanachama wa Agora, ambao watakuwa kutoka taaluma zifuatazo:

  • Wataalam wa vyombo vya habari - watangazaji, watangazaji wa vipindi, waigizaji, watayarishaji, nk., kutoka runinga, redio, magazeti, au filamu.
  • Wachekeshaji
  • Damisi, wasanii, na waigizaji bubu wa kitaalam.
  • Waandishi wa hadithi za kubuni.
  • Waandishi wa habari
  • Wazungumzaji wataalam kutoka mzunguko wa wazungumzaji wa mbele ya hadhira (wanaolipwa).
  • Wazungumzaji kutoka matukio mengine ya uzungumzaji wa mbele ya hadhira kama vile TEDx., Munk Debates, nk.


Alama za Hotuba

Majaji watatoa alama za hotuba kulinganan na vigezo vifuatavyo:

  • Uhalisia (0 mpaka 10)
  • Utumiaji wa lugha (0 mpaka 10) - Watazingatia utajiri, maelezo, na uwazi wa lugha ambayo imetumiwa.
  • Utumiaji wa lugha ya mwili (0 mpaka 10) - Watazingatia utajiri na uonyeshwaji wa lugha ya mwili ya mzungumzaji na kama inaimarisha maudhui ya vichekesho na kama zina muingiliano na simulizi.
  • Utumiaji wa zana au visaidizi vya kuona (0 mpaka 10) - Watazingatia ufanisi wa visaidizi vya kuona au zana kwenye kukuza ucheshi wa hotuba.
  • Maudhui ya kuchekesha (0 mpaka 10) - Watazingatia ni jinsi gani hotuba ilikuwa inachekesha.
  • Mwitikio wa hadhira (0 mpaka 10) - Watazingatia jinsi gani hadhira wameitikia ucheshi/vichekesho vya mzungumzaji.

Kwa kila hotuba, wastani wa kila alama za hapo juu utatafutwa, na hiyo ndio itakuwa alama ya mwisho atakayopewa mshiriki.

KUMBUKA: Utumiaji wa zana au visaidizi vya kuona ni wa hiari. Kama mshiriki hakutumia zana au visaidizi vya kuona vyovyote, kipengele hiki kitatolewa kwenye kutafuta wastani wa alama.

Cheo

Mshindi wa ngazi yoyote isipokuwa Fainali za Dunia atakuwa na cheo cha "Mzungumzaji Bora wa Vichekesho wa (kanda)”

 


Contributors to this page: zahra.ak and agora .
Page last modified on Saturday August 21, 2021 10:00:16 CEST by zahra.ak.